Luke 9:10-15

10 aMitume wake waliporudi, wakamweleza Isa yote waliyofanya. Akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji uitwao Bethsaida. 11 bLakini umati wa watu ukafahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.

12 cIlipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”

13Isa akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”

Nao wakajibu, “Hatuna zaidi ya mikate mitano na samaki wawili. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.”
14Walikuwako wanaume wapatao 5,000.

Isa akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini hamsini.”
15Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote.
Copyright information for SwhKC